top of page

PATA MAARIFA KUHUSU VITU VINAVYOWEZA KUKUONGEZEA FAIDA KWENYE KAZI YA UFUGAJI.

  • Writer: ReSta AgroVET
    ReSta AgroVET
  • Jul 4, 2018
  • 4 min read

Updated: Jul 5, 2018



(AI) UHIMILISHAJI/ Artificial Insemination*

inajulikana kwa wafugaji wengi kama AI, ni moja ya mbinu za kuzaliana ambazo zimechangia katika maendeleo ya sekta mifugo hasa katuka sekta ya maziwa katika nchi zilizofanikiwa kwenye ufygaji wenye tija na faida kubwa.

Mbinu ya AI  huanza na kuchagua ng'ombe wenye afya nzuri, ambao hawana ugonjwa wala kilema cha aina yoyote na wenye uwezo wa kuzalisha mazoa yake kwa kiasi kikubwa cha ubora wa juu. Wafugaji/ Wakulima wanashauriwa kutumia mbegu zilizothibitika kutoka kwa mifugo wazazi walio thibitika ambao wanapatikana kutoka vituo vya AI na watoa huduma waliosajiliwa.

✅ *Faida za Uhimilishaji/AI* 1.Kuzuia magonjwa yanayoweza kuenezwa kutoka kwa dume.

2.Kiasi cha mbegu nyingi kinaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu na kwa gharama ndogo ili kuwezesha upimaji mkubwa na uteuzi wa ng'ombe bora.

3.Inaimarisha na kuboresha maendeleo na ubora wa  maumbile kwa sababu ng'ombe bora zaidi huchaguliwa na hutumiwa kukusanya mbegu.

4. Wafugaji/wakulima wadogo wadogo kwa njia ya AI wanaweza kupata ng'ombe wazuri kwa bei nafuu 5. Mfugaji Unaweza kuchagua ng'ombe mwenye sifa unazozitaka.

6. Ni rahisi kudhibiti tatizo la inbreeding(wanyama wa koo moja kuzaliana kaka na dada) kwa mifugo.

7. Inasaidia kuongeza thamani na kipato kwa mfugaji ataboresha mifugo yake na  mazao yatokanayo na mifugo na kuuza kwa bei nzuri.

✅  *Hasara za AI/Uhimilishaji*

1.Inahitaji maarifa ya kutambua mnyama ambaye yuko kwenye joto na muda  unaofaa wa kupandikiza mbegu  ili kupata uhakika mkubwa zaidi wa kushika mimba na kuzaliwa.

2. Wahamishaji lazima wawe na mafunzo juu ya mbinu hii.

3. Inahitaji uwekezaji mkubwa katika vifaa.

*Sababu zinazoathiri kiwango cha mimba na kuzaliana kwa mbinu ya AI:*

Mnyororo wa uzazi/kuzaliana hutegemea kutungwa kwa mimba na kuzaa kiumbe mwenye afya. Ili Mimba  itungwe inategemea mambo kadhaa, ambayo huunda mnyororo wa kuzaliana/uzazi. Dhana ya mnyororo ni kwamba tunazungumzia uwezo wa viungo vya mwili wa mnyama.  kama kiungo  kimoja kikiwa na shida Kwa hiyo kwenye mnyororo wa kuzaliana kutaathirika na kuathiri kutungwa kwa mimba na uwezo wa kuzaa.

✅ *Sababu zinazoathiri uzalishaji kwa ng'ombe wa maziwa*

Imekuwa ni kawaida kwa wafugaji wengi wa ng'ombe wa maziwa kutofautiana katika kiwango cha uzalishaji kutoka shamba hadi shamba na wanyama kwa wanyama. Tofauti hii ya uzalishaji inaweza kuboreshwa kwa kutumia mbinu za kitaalam kama AI ili kuboresha ng'ombe na mazao yatokanayo na mifugo

Sababu zinazohusiana na kutofikia malengo ya uzalishaji wa maziwa. 1⃣.Sababu zitokanazo na wanyama wenyewe:*

☑ *Jamii na koo za mnyama* - Uwezo wa uzalishaji wa maziwa hupungua kama ifuatavyo - Friesian, Ayrshire, Guernsey, Jersey, Sahiwal, Boran na Zebu. Hii inatokana na maumbile Ya Genetic ya koo za mnyama.

☑ *Uhusiano wa umri wa ng'ombe*

- Ng'ombe  wakubwa zaidi ya  (>miaka  6 ) wanazalisha maziwa 25% zaidi kuliko ng'ombe wadogo kiumri. Uzao wa Kwanza first lactation huzalisha maziwa 25% chini zaidi ya fourth lactation uzao wa nne. Pia Baada ya mavuno ya kuzalisha maziwa mengi  peak lactation kuna kushuka kwa kiasi cha uzalishaji, kutikana na ng'ombe kuingezeka umri na kuzeeka.

Hivyo mfugaji unashauriwa kipindi ambacho  uzalishaji wa maziwa unaongezeka kwa umri, shamba la ng'ombe hupaswa kuwa na wanyama wadogo ili kuboresha uzalishaji na kuwabadilisha ng'ombe waliozeeka.

 ☑ *Stage/Hatua ya uzalishaji Hatua ya uzalishaji wa maziwa stage of lactation*- Uzalishaji wa maziwa huongezeka wakati wa miezi miwili ya kwanza kufuatia kuzaliwa kwa ndama/calving (uzalishaji kufikia kilele), kisha hupungua hatua kwa hatua baadaye.

☑ *Oestrus/siku za joto* uzalishaji wa maziwa hupungua siku ambayo ng'ombe yupo  joto au siku baada ya joto.

☑ *Mimba/Pregnancy stage-*  Kwa ng'ombe mwenye mumva ya miezi 4 hadi mwezi wa 5 wa ujauzito, uzalishaji wa maziwa  wa ng'ombe hupungua kwa kasi zaidi.

☑ *Ukubwa wa ng'ombe*- Ng'ombe wenye maumbile makubwa huzalisha maziwa zaidi kuliko ng'ombe wadogo wa uzao sawa na koo moja.

✅ *Sababu zinazotikana na mazingira:*

☑ *Malisho*- Lishe ni muhimu sana na upungufu wa virutubisho, hasa protini au nishati hupunguza uzalishaji wa mazao ya maziwa. Urefu wa kipindi ambacho ng'ombe hupunzishwa kukamuliwa.(dry period) Kupumzisha kwa Kipindi cha muda mfupi chini ya siku (<60days) husababisha uzalishaji wa maziwa kushuka. Hali ya ng'ombe wakati wa kuzaa - Ng'ombe waliokonda sana au  walionenepa na mafuta mengi huzalisha maziwa kidogo.

☑ *Ratiba ya ukamuaji maziwa*- Ng'ombe wanaokamuliwa mara 3 wanazalisha maziwa zaidi ya asilimia 10-25% kuliko wale wanaokamuliwa mara mbili kwa siku.  Pia Ng'ombe wanaokamuliwa mara 4kwa siku huzalisha zaidi ya 5-15% za maziwa  walewanaokamuliwa maziwa mara tatu.

☑ *Mpangilio wa Shamba* - Uhusiano wa mpangilio wa malisho, sehemu ya kukamulia,  seheme ya banda na sehemu ya maji. Wanyama wanaotembea umbali mrefu watatumia nguvu/energy nyingi, ambayo wanapaswa kutumia kwa ajili ya kutengeneza maziwa.

☑ *Magonjwa* - Magonjwa kama ya kiwele Mastitis, milk fever na mengine huathiri uzalishaji wa maziwa. Mabadiliko ya mkamuaji na utaratibu wa ratiba ya ukamuaji maziwa husababisha kupungua maziwa.

☑ *Hali ya hewa/Climate* - joto kali la juu hupunguza mavuno ya uzalishaji maziwa zaidi kuliko joto la chini. joto huathiri raha ya wanyama na ulaji wa chakula.

Mifugo iliotoka kwenye mazingira ya baridi huathiriwa zaidi na joto kuliko mifugo iliyozoea mazingira ya joto. Hivyo mfugaji unashauriwa kufahamu vizuri jamii na aina ya ng'ombe unaotaka kuwafuga waendabe na mazingira halisi ili kuleta tija. .  #Written by Dr Riziki Ngogo _____________________________________________

Jifunze mengi Fuga na  ReSta AgroVET tupo Morogoro/ Msamvu kidabaga/Mtaa wa genda/ karibu na ATM za CRDB.  Kwa daladala shuka kituo cha polisi msamvu barabara mpya ya kichangani yenye mataa iliyopo oposite na the islamic foundation Radio Imamu 0763222500 0652515242 _________________________________

The Recommended Standards for all your Animal Care needs, Veterinary Services and Products.  Pata vitabu vya mwongozo bora ufugaji wenye tija hatua kwa hatua.

__________________________________ #Fuga kwa Muda mfupi Uza Fuga tena. #Tumia gharama kidogo pata faida kubwa. #Jipatie kitabu kinachokupa maarifa sahihi. #Fuga kwa tija hatua kwa hatua SOMA FUGA TAJIRIKA..... __________________________

KARIBU!  ReSta AgroVET Sasa Unaweza kupata huduma zetu zote za mifugo kutoka kwa wataalam wetu waliosajiliwa popote ulipo tunakufikia.

Comments


Vifaranga & kuku wakubwa

Ongea na Daktari​

Chanjo na Kinga !

Get your lovely puppy

for pet and security dog lovers

Farm and housing structure​

Ujenzi wa mabanda kulingana na mifugo.

Ufugaji wa Samaki kibiashara​

Zingatia ujenzi wa mabwawa na mambo muhimu.

Cages na Vifaa muhimu​

Jipatie pembejeo zote za muhimu.

© 2018 ReSta AgroVET Tanzania. 0763222500/ 0652515242, The Recommended Standard for All your Animal Care needs, Veterinary  Services and Products.

bottom of page